We exist to close the gap in mental health awareness across Swahili-speaking communities. Clear, trusted information about depression, anxiety, trauma or a child's behaviour is not always easy to find in Kiswahili. Each episode takes one topic and explains it in plain language.Tupo ili kuziba pengo la uelewa wa afya ya akili katika jamii zinazozungumza Kiswahili. Taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu sonona, wasiwasi, kiwewe au tabia za mtoto si rahisi kila mara kuzipata kwa Kiswahili. Kila kipindi huchukua mada moja na kuieleza kwa lugha rahisi.
Our content is evidence-based and made with clinical psychologists, psychiatrists and other medical professionals. We add practical tips and advice listeners can use, and we invite the community into the conversation.Maudhui yetu yanategemea ushahidi na hutayarishwa pamoja na wanasaikolojia tiba, madaktari bingwa wa magonjwa ya akili na wataalamu wengine wa afya. Tunaongeza vidokezo na ushauri wa vitendo ambao wasikilizaji wanaweza kuutumia, na tunaikaribisha jamii kushiriki mjadala.
We believe people should be able to talk about their minds without shame. That means lowering the barriers to information, reducing stigma, encouraging peer support, and helping every listener take an active role in their own wellbeing.Tunaamini kila mtu anapaswa kuzungumzia akili yake bila aibu. Hii inamaanisha kupunguza vikwazo vya kupata taarifa, kupunguza unyanyapaa, kuhamasisha msaada wa rika, na kumsaidia kila msikilizaji kuchukua hatua kwa ustawi wake mwenyewe.
Mending Thoughts is produced by AYYA, Inc., a mental health organisation based in Dar es Salaam, working to make care easier to reach across Africa.Mending Thoughts inatayarishwa na AYYA, Inc., shirika la afya ya akili lenye makao yake Dar es Salaam, linalofanya kazi ya kurahisisha upatikanaji wa huduma barani Afrika.